IVO MAPUNDA ATOA MAZITO KWA TIMU YA TAIFA YA SERENGETI BOYS

IVO Mapunda kipa aliyedakia timu zote kubwa nchini zikiwemo Simba, Yanga na Azam, amewataka nyota wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Vijana "Serengeti Boys" kuacha kubweteka na matokeo ya kirafiki ambayo wanayapata.

Kipa huyo mkongwe alisema kuwa Serengeti Boys bado wana kazi kubwa nchini Gabon na isingekuwa vema kama wataanza kulewa sifa mapema na kusahau jukumu lililowapeleka.

“Kikosi kinaonekana kuwa na maendeleo mzuri wa matokeo ya mechi za kirafiki lakini hiyo isiwe sababu ya kuridhika na mafanikio kiduchu, wanapaswa kujua Gabon kuna kazi kubwa,” alisema Ivo.

“Watanzania wote macho yapo kwao ndiyo maana unaweza kuona jinsi ambavyo watu wanajitosa kuchangia, timu ya Taifa ina uhaba wa Mataji na wao wamepewa dhamana hawapaswi kuzembea hata kidogo."


Michuano ya Africon kwa vijana inatarajia kuanza Mei 14 mwaka huu ambako Serengeti Boys iliweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kufanya maandalizi na imecheza mechi ya kirafiki na mwenyeji Gabon na kupata ushindi wa mabao 2-1.

Labels: