Waimbaji nyota wa taarab Sabah Muchacho na Jokha Kassim, Jumamosi
usiku walikuwa kivutio kwenye onyesho la Jahazi Modern Taarab ndani ya ukumbi
wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Nyota hao wawili walikuwa waalikwa kwenye onyesho hilo lililopewa jina
la “Usiku wa Ustaarabu wa Pwani”.
Jokha akapanda na kete mbili “Utakufa Nacho” na “Domo la Udaku” huku
Sabah akitisha na “Fumbo” na “Wa Mungu U Wazi”.
Mbali na nyota hao, Jahazi nao walikamua show ya maana huku umati
uliofurika Dar Live ukiselebuka mwanzo mwisho.
Fatma Kassim
Jokha Kassim
Jokha akipagawisha na "Domo la Udaku"
Jumanne Ulaya kwenye solo gitaa
Ally Jay akipapasa kinanda kwa mbwembwe
Mtu na dadake ...Fatma Kassim na Jokha Kassim
Sabah Muchacho
Malkia Leyla Rashid (kulia) alikuwepo ukumbini kushuhudia onyesho hilo na hakusita kwenda kumtunza Sabah
Prince Amigo kwenye anga zake
Amigo akiendelea kuwajibika
Ukumbi 'ulitapika' kama hivi
Mwasiti Mbwana Kitoronto akiimba "Nataka Jibu"
Twaha Malovee ambaye kwasasa anaitumikia Msondo Ngoma, alipanda na kuimba wimbo "VIP"
Zubeida Mlamali
Hadija Mbegu chipukizi anayekuja kwa kasi Jahazi
Labels: MUZIKI