Katika chombo ambacho kinaonekana hakina muhisika kamili katika Twanga
Pepeta, ni tumba ambazo zimekuwa chachu ya muziki wa bendi hiyo tangu albam ya
“Fainali Uzeeni”.
Katika albam za “Kisa Cha Mpemba” na “Jirani” tumba ndani ya Twanga
Pepeta kilikuwa chombo ‘msindikizaji’ ambacho hakikupewa umuhimu mkubwa na
kilikuwa kikipwa kiujanja ujanja na marehemu Banza Stone na wakati mwingine
hata mwimbaji wa kike Jesica Charles.
Lakini tangu ujio wa marehemu MCD mwanzoni mwa miaka ya 2000, tumba za
Twanga zikapata heshima kubwa na kuwa na mvuto wa kipekee kwenye muziki wa
bendi hiyo.
Kwa bahati mbaya sana, tumba za Twanga zinarejeshwa tena katika enzi
za “Kisa cha Mpemba” na “Jirani” ambapo sasa chombo hicho hakina wenyewe na
kinapigwa na kila mtu, hata mashabiki wanapanda na kuzipiga.
Katika onyesho la Jumamosi ndani ya Mango Garden, tumba za Twanga
zilipigwa na watu sita tofauti – Kirikuu, Maga, Joshua, Thabit Abdul, Mandela
na shabiki mmoja ambaye jina lake halikupatikana. Ilikuwa kama vile jamvi la
wageni, yeyote analikalia.
Hata hivyo, habari njema ni kwamba meneja mpya wa Twanga Martin
Sospeter ameimbia Saluti5 kuwa wanatafuta mpiga tumba mpya.
Martin amesema kwa yeyote mwenye uwezo wa kupiga
tumba awasiliane naye kupitia namba 0715202888.
Hapa tumba za Twanga zikipigwa na Thabit Abdul
Hapa zinapigwa na mwimbaji Joshua
Hapa ilikuwa zamu ya tumba kupigwa na mpiga drum Kirikuu
Dansa Maga naye akionyesha mbwembwe zake kwenye tumba
Dansa Mandelea naye hakubaki nyuma
Mdau huyu wa muziki ambaye jina lake halikupatikana ndiye aliyekuwa akipanda mara nyingi kupiga tumba za Twanga Jumamosi usiku
'Kipofu' na 'chongo' ...hapa wawili hawa walikuwa wakifundishana namna ya kupiga tumba
Labels: MUZIKI