Jumamosi iliyopita ‘kilinuka’ kwenye
ukumbi wa Airport Pub mjini Morogoro pale Jahazi Modern Taarab walipoangusha
burudani iliyokwenda shule.
Mashabiki wa Morogoro waliojazana ukumbini
humo, walipagawa na kila wimbo wa Jahazi, wakacheza bila kuchoka kuanzia mwanzo
wa show hadi mwisho.
Waimbaji Mwasiti Kitoronto, Mariam
Kasola, Mishi Zere, Fatma Kassim, Hadija Mbegu, Zubeida Mlamali na Prince Amigo
waliacha heshima kubwa Morogoro kwa namna walivyojua kucheza na hadhira ya
mashabiki.
Ally Jay akionyesha ubora wake wa kupapasa kinanda
Prince Amigo akisema na kijiji
Emeraa akikamu gitaa la solo
Mwimbaji Fatma Kassim
Hadija Mbegu mwimbaji kiraka wa Jahazi
Jumanne Ulaya "J Four" na gitaa lake la solo
Mbwembwe kama hizi huja pale show inapofana kinoma ...Mishi huyo!!
Mishi Zere akiwa kwenye safu ya waimbaji wa Jahazi
Prince Amigo "Bosi kichefuchefu" akiwapa raha wakazi wa Morogoro
Amigo akiendeleza makamuzi
Mishi na wimbo wake "Nia Safi Hairogwi"
Mishi na Jumanne Ulaya
Shomari Zizzou alifunika sana na bass lake
Labels: MUZIKI