MREMBO Mariah Carey amesema kuwa muziki ndio kazi pekee iliyompa kila kitu alichowahi
kukiota miaka ya nyuma kabla ya kuwa staa mkubwa.
“Nina
hisia kama wanadamu wengine ambao wanastahili heshima katika jamii, lakini
nakiri kuwa ndoto zangu nyingi zimetimia tangu nianze kujihusisha na masuala ya
muziki, alisema staa huyo.
“Kuna
wakati huwa najiuliza kama sio muziki ningekuwa wapi kwasababu naona mafanikio
yangu yametokana na kazi hii,” aliongeza Mariah Carey.
“Nimezunguuka
karibu kila pande ya dunia kwasababu ya kazi hii na sikuwahi kufikiri kama
inaweza kunifikisha hapo nilipo, nimekuwa nikiwaza muziki wakati wote,”
alimaliza.
Labels: MUZIKI