Bendi ‘mpya’ ya Mapacha Watatu chini ya Khalid Chokoraa, Jumapili
iliyopita, iliwasha moto wa burudani ndani ya ukumbi wa Garden Breeze, Magomeni
Mapipa jijini Dar es Salaam.
Mapacha Watatu iliyokuwa na sura za wasanii wa kukodiwa kama na Said
Ndagendage mpiga Kinanda wa Zanzibar Stars Modern Taarab, mwimbaji/rapa Frank
Kabatano na mpiga bass Evans Mwaigomole wote kutoka TOT, ikatesa kwa program ya
nyimbo mchanganyiko - za ndani na nje ya nchi.
Chokoraa akitengeneza safu ya uimbaji sambamba na Catty Chuma na
January Elevan ambao wote waliwahi kushiriki na Mapacha Watatu ile ya mwanzo, wakafanikiwa
kupiga nyimbo zote kali za Mapacha wakifukia vizuri sauti za Jose Mara na
Kalala Jr.
Mbali na nyimbo za dansi, Mapacha Watatu iligonga hadi nyimbo za
taarab ambapo wimbo “Njiwa Peleka Salamu” wa JKT Taarab, ulitendewa haki na
Catty Chuma.
Kwenye drum alikuwepo Martin Kibosho, solo likashikiliwa na Super
Black, safu ya wanenguaji ikaundwa na Sabrina, Otilia na Master B.
Lakini kubwa zaidi ni kwamba Chokoraa ambaye aliahidi kutotumia
wasanii wa Twanga Pepeta, mbali na kukiuka kali yake kwa kuwachukua Otilia na
Master B, pia amemjumuisha Amani “Rasi”, kijana anayetoka ndani kabisa ya
familia ya kina Asha Baraka.
Amani kwa miaka mingi alikuwa ndiyo mtu anayesimama getini kwenye show
za Twanga Pepeta na kupokea tiketi, lakini Chokoraa alimjumuisha katika show
yake ya Jumapili na kumtupa kwenye safu ya waimbaji wa Mapacha Watatu. Kipaji
kipya kimevumbuliwa.
Evans kwenye gitaa la bass
Catty Chuma kwenye safu ya uimbaji
Khalid Chokoraa boss wa Mapacha Watatu
Catty Chuma "First Lady"
Sabrina mmoja wa madansa wa Mapacha Watatu
Amani "Rasi" akiunda safu ya waimbaji wa Mapacha Watatu
January Eleven na Chokoraa
Frank Kabatano
Martin Kibosho kwenye drums
Ndagendage kwenye kinanda
Sabrina na Otilia
Otilia, Sabrina, Master B kwenye safu ya unenguaji
Super Black kwenye solo. Nyuma yake ni fundi mitambo Masoud ambaye pia hutumiwa na Twanga Pepeta
January Eleven akiimba kwa hisia kali
Labels: MUZIKI