Bendi tatu za taarab Jahazi Modern Taarab, Yah TMK na Wakali Wao
Jumapili usiku zilichuana vikali kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni,
jijini Dar es Salaam.
Hakuna bendi iliyokubali kuwa ‘mnyonge’ kwani kila moja ilihakikisha
inaweka silaha zake za maangamizi kwa kuchagua nyimbo zinazokubalika zaidi.
Bendi hizo zilichuana kwa mfumo wa kupokezana ambapo kila bendi
ilirudi jukwaani mara mbili.
Wakali Wao iliyokuwa chini ya mtunzi na mtengenezaji mahiri wa muziki,
Thabit Abdul, ndio iliyokufungua pazia la burudani katika kila mzunguko.
TMK inayojengwa na wapiga vyombo tishio, yenyewe ilikuwa ya pili
katika kila mzunguko huku Jahazi inayobebwa na utajiri wa nyimbo zenye
kukubalika na kufahamika zaidi ndiyo iliyokuwa ihitimisha mpambano huo.
Wakati Jahazi nyimbo zao zote zilitesa katika kila mzunguko, bendi
nyingine zilitesa kwa baadhi nyimbo.
Mwitikio wa mashabiki ulikuwa ni mzuri na wa kuridhisha kulingana na
hali ya uchumi kwa sasa.
Aisha Mtamu Kabisa wa Wakali Wao akiimba "Thamani ya Pendo"
Aisha Vuvuzela wa Yah TMK akiimba wimbo "Kibaya Kina Wenyewe" ambao ulikubalika sana
Amina Mnyalu wa Yah TMK
Fatma Mcharuko mmoja wa waimbaji waliotikisa Travertine
Hadija Mbegu wa Jahazi
Jumanne Ulaya kwenye mpini wa solo wa Jahazi
Mwasiti Kitoronto wa Jahazi
Rahma Machupa wa Wakali Wao na wimbo wake "Yataka Moyo"
Mariam BSS wa Jahazi akiimba "Nipe Stara"
Mohamed Mauji akicharaza solo la Yah TMK
Mauwa Teggo wa Yah TMK
Mwasiti alikuwa MC kwa upande wa Jahazi
Fatma Mcharuko akitesa na "Siwaguni Siwakohoi"
Miriam Amour wa Wakali Wao
Miriam Amour
Mishi Zele wa Jahazi akiimba "Nia Safi Hairogwi", namba nyingine iliyotikisa Travertine
Mishi Zele akiimba kwa kujiamini
Aisha Mtamu Kabisa wa Wakali Wao mmoja wa waimbaji waliofanya vizuri
Mwimbaji Mohamed Ali "Mtoto Pori" wa Wakali Wao
Mtoto Pori
Fatma Mcharuko wa TMK akimtunza Mwasiti Kitoronto wa Jahazi
Hali ilivyokuwa Jumapili usiku
Omar Teggo akiimba "Figisu Figisu"
Omar Teggo kutoka Yah TMK
Amigo wa Jahazi katika ubora wake
Rahma Machupa wa Wakali Wao
Muddy K (kushoto) na Said Fella
Thabit Abdul akipapasa kinanda cha Wakali Wao
Prince Amigo wa Jahazi
Umati uliofurika Travertine
Aisha Vuvuzela wa Yah TMK
Wadau wakifuatilia onyesho kwa makini
Waimbaji wa Jahazi
Hadija Mbegu wa Jahazu akisepa na kijiji
Waimbaji wa Wakali Wao
Labels: MUZIKI